Wednesday, March 26, 2014

ALJEBRA MAFUMBO A1Mwalimu aligawa kalamu 600 kwa wanafunzi wake kama ifuatavyo: Rama alipata mara tatu ya Juma, wakati Ana alipata mara mbili ya Rama. Je Ana alipata kiasi gani?

Suluhu

Tunachora jedwali dogo ili uelewe namna ya kufanya swali hili.

Rama
Juma
Ana
Jumla ya kalamu
3(x) = 3x
x
2(3x) = 6x
600

3x + x + 6x = 600

10x = 600

10x = 600
10      10

x = 60.

Kalama alizopata Ana;

= 6x

=6(60)

=360

Hivyo Ana alipata kalamu 360.


ZAMU YAKO………………….

Mateo aligawa matofali 3200 kwa watoto wake kama ifuatavyo: Bob alipata mara tano ya Dani, wakati Kim alipata mara mbili ya Bob. Je Kim alipata kiasi gani?

SEHEMU MAFUMBO A1Kisoso alitumia 3/5 ya pesa yake kununua nyanya. Tafuta kiasi kilichobaki Ikiwa alikuwa na sh. 10,000.

Suluhu

= 3 x 10,000
  5

= 3 x 10,0002000
  5

= 3 x 2000

= 6000

Kiasi kilichobaki = 10,000 – 6000
                            = 4000/=

Hivyo alibakiwa na sh 4000/=.


ZAMU YAKO………………….

Mligo alitumia 3/8 ya pesa yake kununua viatu. Tafuta kiasi kilichobaki Ikiwa alikuwa na sh. 32,000.

UWIANO A5Marwa aligawa sh 12,000/= kwa watoto wake watatu katika uwiano wa 2:7:3. Tafuta kiasi alichopata motto wa pili.

Suluhu

Kwanza tunajumlisha uwiano: 2 + 7 + 3 = 12
Mtoto wa pili ana uwiano wa 7. 

sehemu ya mtoto wa pili ni 7/12.

Mtoto wa pili = 7  x  12,000
                        12
Mtoto wa pili = 7  x  12,0001000
                        121
Mtoto wa pili = 7  x  1000

Mtoto wa pili = 7,000.


Hivyo mtoto wa pili alipata 7000/=


ZAMU YAKO…..

Chacha aligawa sh 16,000/= kwa watoto wake watatu katika uwiano wa 2:5:3. Tafuta kiasi alichopata motto wa pili.

ALJEBRA A23Tafuta y Ikiwa 11y – 8 = 5y + 10.

Suluhu

11y – 8 = 5y + 10

11y - 5y = 8 + 10  (baada ya kukusanya mitajo inayo fanana)

6y = 18

6y = 18
6      6

y = 3


ZAMU YAKO……………….

Tafuta y Ikiwa 10y – 20 = 3y + 8.

KDS A13
Tafuta KDS cha 30 na 66.

Suluhu      


2
30
66
3
15
33
5
5
11
11
1
11

1
1


KDS = 2 X 3 x 5 x 11

       = 330

Hivyo KDS ni 330


ZAMU YAKO……………….

Tafuta KDS cha 40 na 66