Monday, February 15, 2016

ENEO LA MSAMBAMBA-1



Tafuta eneo la msambamba ufuatao.




Solution


Eneo = kitako  x  kimo

       = 13 x 5

       = 65


Hivyo eneo ni sm2 65.

ZAMU YAKO………………


Tafuta eneo la msambamba ufuatao.





ALGEBRA - 8


Ikiwa   1m  =  7; tafuta m.
             3

Suluhu

1m  =  7
3

13 x 1m  =  7 x  3     zidisha kwa 3 kila upande
        13

1m = 7 x 3

m = 21

Hivyo m = 21


ZAMU YAKO……………..

Ikiwa   1e  =  5;  tafuta e.
            10






MAFUMBO-2



Mayanja ana machungwa 900. Alikula machungwa 125. Je alibakiwa na machungwa mangapi?

Suluhu

Hapa tunatakiwa kutoa:
                    

JUMLA
Mayanja
   900
-  125
Alikula
BAKI
   775

Hivyo alibakiwa na machungwa 775


ZAMU YAKO………………


Nyamwaga alinunua penseli 760. Aliwagawia watotowake penseli 136. Je, alibakiwa na penseli ngapi?


Saturday, February 13, 2016

MAFUMBO-1


Mayanja ana magari 400. Kasita ana magari 700. Je, jumla wana magari mangapi?

Suluhu

Hapa tunatakiwa kujumlisha:
                    


JUMLA
Mayanja
  400
+700
Kasita
JUMLA
1100

Hivyo jumla ya magari yao ni 1100


ZAMU YAKO………………



Malima ana magari 600. Kasimu ana magari 800. Je, jumla wana magari mangapi?

UJAZO - 1


Tafuta kimo cha mche mstatili ufuatao ikiwa ujazo wake ni  sm3420



Suluhu

Ujazo = urefu x upana x kimo


420 = 10 x 7 x h


420 = 70 x h


420 = 70h
 70      70
 
6 = h

Kwa hiyo kimo ni sm 6.


ZAMU YAKO………………

Tafuta kimo cha mche mstatili ufuatao ikiwa ujazo wake ni  sm3240




ALGEBRA - 7


Ikiwa 4a + 20 = 44; tafuta thamani ya a

Suluhu

4a + 20 = 44

4a + 20-20 = 44-20  [toa 20 kila upande]

4a + 0 = 24

4a = 24

4a = 24                    [gawa kwa 4 kila upande]
4       4

a= 6

Kwa hiyo a = 6

ZAMU YAKO………………


Ikiwa 4m - 20 = 24; tafuta thamani ya m


Friday, February 12, 2016

NYUZI - 2


Tafuta thamani ya G katika umbo lifuatalo.



Suluhu

Jumla ya nyuzi za mstari mnyoofu ni 1800

G + 650 = 1800

G= 1800 - 650

G = 1150

Hivyo thamani ya G ni 1150


ZAMU YAKO………………



Tafuta thamani ya G katika umbo lifuatalo.





ALGEBRA - 6


R - 11 = 2. Tafuta thamani ya R.

Suluhu

R - 11 = 2

R – 11 + 11 = 2 + 11

R – 0 = 13

R = 13


Hivyo R = 13


ZAMU YAKO………………


w - 8 = 7. Tafuta thamani ya w.


UMRI - 1


Umri wa Kaisari ni mara nne ya ule wa Maneno. Ikiwa jumla ya umri wao ni miaka 65, Tafuta umri wa wote.

Suluhu

Kaisari = t

Maneno = 4t

Kaisari
Maneno
Jumla
t
4t
65

t+4t = 65

5t = 65

5t = 65
5       5

t = 13

Umri wa Kaisari = t

                          = 13


Umri wa Maneno = 4t

                            = 4 x 13

                            = 52


Hivyo umri wa Kaisari ni miaka 13 na ule wa  Maneno ni miaka 52


ZAMU YAKO………………


Umri wa Kikwete ni mara tano ya ule wa Riziwani. Ikiwa jumla ya umri wao ni miaka 80, Tafuta umri wa wote.

Thursday, February 11, 2016

MZINGO WA MRABA - 1


Tafuta mzingo wa mraba ufuatao





Solution


Mzingo = 4  x  upande

              = 4 x 33

              = 132



Hivyo mzingo ni sm 132.



ZAMU YAKO………………



Tafuta mzingo wa mraba ufuatao










ALGEBRA - 5


Ikiwa 4u + 8 = 32; tafuta thamani ya u.


Suluhu


4u + 8 = 32


4u + 8-8 = 32-8   {toa 8 kila upande}


4u + 0 = 24  {kwa sababu 8-8 = 0}


4u = 24


4u = 24            {gawa 4  kila upande}
4       4

u= 6


Kwa hiyo u = 6


ZAMU YAKO………………



Ikiwa 2x + 10 = 32; tafuta thamani ya x.

ALGEBRA - 4


Ikiwa  3w = 28; tafuta thamani ya w

Solution

3w = 28

3w = 28          [gawanya kwa 3 kila upande]
3        3

w = 91/3 


Hivyo w = 91/3  

ZAMU YAKO………………


Ikiwa  5a = 39; tafuta thamani ya a.

Wednesday, February 10, 2016

NYUZI - 1



Tafuta m kwenye umbo lifuatalo.



Suluhu

3m + m + 960 + 1080 = 3600

4m + 2040 = 360 [baada yakukusanya mitajo inayofanana]

4m = 3600 - 2040

4m = 1560

4m = 1560       [gawa kwa 4 kila upande]
4        4

m = 390



ZAMU YAKO………………


Tafuta a kwenye umbo lifuatalo.





MAGAZIJUTO - 1



Kokotoa 50 ÷ 2 – 7.

Solution

Tutatumia MAGAZIJUTO.

Kwanza i) gawanya 
             ii) halafu utoe


= 50 ÷ 2 – 7.

= 25 - 7 [baada ya kugawanya].

= 18  [baada ya kutoa].


TRY THIS…………


Kokotoa 70 ÷ 2 – 5.


ALGEBRA - 3


Tafuta y Ikiwa 23y – 8 = 9y + 20.

Suluhu

23y – 8 = 9y + 20

23y - 9y = 8 + 20  (baada ya kukusanya mitajo inayo fanana)

14y = 28

14y = 28
14     14

y = 2


ZAMU YAKO……………….


Tafuta w Ikiwa 8w – 20 = 3w + 15.