Tuesday, May 27, 2014

SIMU YA MAANDISHI A2



Kampuni ya simu hutoza shilingi 600 kwa maneno kumi ya mwanzo, na sh 80 kwa kila neno linaloongezeka. Tafuta gharama ya kutuma maneno 16.

Suluhu

Maneno 16 – maneno 10 ya mwanzo = maneno 6 yanayoongezeka.
Maneno 6 x sh 80 = sh.480
Jumla ya gharama = maneno 10 ya mwanzo + maneno yanayoongezeka
                             =  600  +  480
                             =  1080

Hivyo gharama ya kutuma maneno 16 ni sh 1080.


ZAMU YAKO……………….

Kampuni ya simu hutoza shilingi 430 kwa maneno kumi ya mwanzo, na sh 70 kwa kila neno linaloongezeka. Tafuta gharama ya kutuma maneno 17.


3 comments: