Wednesday, March 26, 2014

ALJEBRA MAFUMBO A1



Mwalimu aligawa kalamu 600 kwa wanafunzi wake kama ifuatavyo: Rama alipata mara tatu ya Juma, wakati Ana alipata mara mbili ya Rama. Je Ana alipata kiasi gani?

Suluhu

Tunachora jedwali dogo ili uelewe namna ya kufanya swali hili.

Rama
Juma
Ana
Jumla ya kalamu
3(x) = 3x
x
2(3x) = 6x
600

3x + x + 6x = 600

10x = 600

10x = 600
10      10

x = 60.

Kalama alizopata Ana;

= 6x

=6(60)

=360

Hivyo Ana alipata kalamu 360.


ZAMU YAKO………………….

Mateo aligawa matofali 3200 kwa watoto wake kama ifuatavyo: Bob alipata mara tano ya Dani, wakati Kim alipata mara mbili ya Bob. Je Kim alipata kiasi gani?

2 comments: