Wednesday, March 26, 2014

ALJEBRA A23



Tafuta y Ikiwa 11y – 8 = 5y + 10.

Suluhu

11y – 8 = 5y + 10

11y - 5y = 8 + 10  (baada ya kukusanya mitajo inayo fanana)

6y = 18

6y = 18
6      6

y = 3


ZAMU YAKO……………….

Tafuta y Ikiwa 10y – 20 = 3y + 8.

KDS A13




Tafuta KDS cha 30 na 66.

Suluhu      


2
30
66
3
15
33
5
5
11
11
1
11

1
1


KDS = 2 X 3 x 5 x 11

       = 330

Hivyo KDS ni 330


ZAMU YAKO……………….

Tafuta KDS cha 40 na 66

ALJEBRA A22



Rahisisha 60(2k)

Suluhu

 =60(2k)

=60 x 2 x k

=(60 x 2) x k

=(120) x k

=120k

Hivyo 60(2k)=120k


ZAMU YAKO………………

Rahisisha 30(2k)

SIMU YA MAANDISHI A1



Kampuni ya simu hutoza shilingi 500 kwa kila neno katika maneno kumi ya mwanzo, na sh 80 kwa kila neno linaloongezeka. Tafuta gharama ya kutuma maneno 16.

Suluhu

Maneno 16 – maneno 10 ya mwanzo = maneno 6 yanayoongezeka.
Maneno 6 x sh 80 = sh.480

Jumla ya gharama = maneno 10 ya mwanzo + maneno yanayoongezeka
                             =  500  +  480
                             =  980

Hivyo gharama ya kutuma maneno 16 ni sh 980.


ZAMU YAKO……………….

Kampuni ya simu hutoza shilingi 470 kwa kila neno katika maneno kumi ya mwanzo, na sh 70 kwa kila neno linaloongezeka. Tafuta gharama ya kutuma maneno 17.

WASTANI A12



Tafuta wastani wa 19 na 17.
           
Suluhu

17 + 19 = 36

Jumla ya namba = 36
Idadi ya namba = 2

Wastani = Jumla ya namba ÷ Idadi ya namba
                = 36 ÷ 2  
                = 18

Hivyo wastani ni  18


ZAMU YAKO……………….

Tafuta wastani wa 23 na 17.